Marcio Barcellos Maximo alimaliza mkataba wake wa kuinoa Taifa stars (Timu ya soka ya taifa ya Tanzania) mwaka 2010 mwezi wa saba, baada ya kuinoa timu hiyo kwa mafanikio kwa muda wa miaka minne. Kati ya mafanikio yaliyoletwa katika soka la Tanzania na mbrazili huyu ni pamoja na kurudisha mapenzi ya wapenzi wa mpira kwa timu yao ya Taifa.
Haikuwa kazi ndogo hata kidogo kwa mbrazili huyu kuifanya timu hii iwe kipenzi tena cha watanzania, ni juhudi ya hali ya juu iliyopelekea imani ya watanzania kwa timu yao kurejea tena. Na hii ilitokana na ukweli kuwa Taifa stars ikaanza kuwa mpinzani wa kweli mara inapokutana na timu mbalimbali za bara la Africa.
Misingi mikuu ya filosofia ya mwalimu huyu ilikuwa katika kujenga nidhamu ndani ya timu, umuhimu wa wachezaji kuthamini kazi yao hii ikiwa ni pamoja na kuzingatia mazoezi, umuhimu wa kujenga timu ya muda mrefu. Katika kuyafanikisha haya yote Maximo aliweza si tu kwa timu yake kuonyesha mchezo mzuri uwanjani bali pia aliweza kuwatumia vijana wadogo chipukizi kama Jerryson Tegete kwa mafanikio.
Ule msemo usemao usione vyaelea vimeundwa ukawapitia mbali kidogo watanzania na kuona alichofanya Maximo ni kidogo, na wao wanaweza kufanya zaidi. Mashabiki na baadhi ya vyombo vya habari vilivyoibuka na dhana ya uchambuzi wa soka vikaanza kumsakama kocha huyu. Tuhuma za kutokuona mchango wa kocha zikaanza kuvuma kila pembe ya nchi, majina ya baadhi ya makocha wazawa yakaanza kutajwa huku na kule kuwa wanauwezo mkubwa kuliko mbrazili huyu. Visa vikaanza kuingia hadi kwa wachezaji, wachezaji wenye kuonyesha nidhamu mbovu wakakingiwa kifua na watanzania, kana kwamba Maximo anawaonea. Na baadhi ya wachezaji hao wameshindikana hadi leo.
Mengi yamefanywa na kocha huyu ikiwa ni pamoja nakupanda kwa timu yetu katika chati za FIFA, Kuweza kushiriki michuano ya kimataifa ya Africa kwa wachezaji wa ndani. Haya yote hayakutosha watu wakataka aondoke na yeye kweli akaondoka. Leo katika pita pita yangu katika mitandao nimekutana na discussion katika jamii forum, cha kushangaza ni kuwa wachangiaji karibu wote wanalalamika kuwa kuondoka kwa Maximo ilikuwa ni kosa kubwa sana kwa soka la Tanzania. Jionee mwenyewe katika link hii http://www.jamiiforums.com/sports/215516-namkumbuka-sana-marcio-maximo.html

Watanzania Majungu
ReplyDelete