Skip to main content

Makocha wa Tanzania Hamtusaidii

Kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukisikia malalamiko juu ya Kocha Marcio Maximo wa Taifa Stars, malalamiko haya yamekuwa yakiongezeka kutokana na baadhi ya makocha maarufu wa kitanzania nao kuchochea kelele hizi.

Maximo amekuwa akilalamikiwa sana kwa mambo makuu mawili kwa sasa;

1. Kumuacha Golikipa Juma Kaseja Juma
2. Kuwaacha Athman Idd na Haruna Moshi

Limeongezeka jingine la kuwa kamuita kipa namba mbili wa stars katika kikosi cha Taifa.

Naomba kwa upeo wangu mdogo niyaongelee haya matatu.

1. Sidhani kama tiba ya Stars ni Juma Kaseja golini; Juma Kaseja sio Kipa mzuri kiasi hicho inavyodhaniwa. Ninachoweza kusema kwa sasa ni kuwa nyota ya Juma Kaseja inang'aa machoni kwa watanzania na si kwamba ana kiwango kikubwa sana golini. Wanasimba wanasahau kama kuna kipindi walikuwa hamtaki kipa huyu kwa sababu ya kufungwa na huku wakisema yeye ndio chanzo. Simba wanasahau jinsi alivyokuwa akifungwa katika mashindano ya Tusker mwaka ule Kagera sugar ilipoivua Simba ubingwa huo.

Juma Kaseja amekuwa kipa namba moja ya timu ya taifa kuliko makipa wote wanaocheza sasa,kipindi chote hicho ameisaidaje stars? Watanzania wanakumbuka mashindano ya Kagame yaliaofanyika hapa mwaka juzi? Watanzania wanakumbuka jinsi alivyokuwa akifungwa na Mbui Twite? Wanaomlilia Kaseja kuwa ndio kipa bora Tanzania, wamemuona Amani Simba awapo golini? Si kweli kuwa Kaseja ndio tiba ya matatizo ya Tanzania katika soka tuangalie tatizo halisi,na sio kwa kutafuta shortcut. Tatizo letu kubwa lipo katika kukuza vipaji vya magolikipa.

Nenda katika timu yoyote uone kama makipa wanafundishwa ipasavyo; walimu wengi hawatilii mkazo program za magolikipa katika timu zao. sio ajabu kukuta makipa wa timu wakifanya mazoezi peke yao bila mwalimu. Mwalimu anakuwa busy na program zingine za timu kama ufungaji, viungo nk.

2. Hili la akina Athman Idd na Haruna Moshi nalo la kulipigia kelele. Kuna asiyejua nidhamu za wachezaji hawa? Au ndio yale mambo ya mzazi kukana kwa kusema mwanangu sio mwizi ilhali wajua fika tabia ya mwanao. Ni mara ngapi wachezaji hawa wameadhibiwa na vilabu vyao, TFF? na hakuna aliyepiga kelele. Leo wanaadhibiwa na Maximo watu wanakuja juu, au kocha mgeni hana haki ya kuadhibu mchezaji wa Tanzania?Tunafuga ubovu ambao hautusaidii kabisa.

Labda nimalizie kwa kuwakumbusha Makocha wazalendo maamuzi yao waliyoyafanya hapo nyuma ambayo hayana tofauti sana na kile anachofanya Maximo kwa sasa.

S.Mziray: Kocha huyu wakati akiwa kocha mkuu wa timu ya taifa aliwahi kumuita kikosini mchezaji Magadula ambaye alikuwa hajawai kucheza super ligi hata mara moja.

Sunday Kayuni: Aliwahi kumuita kikosini mchezaji Nteze John Lungu ilhali machezaji huyu alikuwa akisotea benchi katika timumyake ya Simba.

Wito wangu kwenu nyote ni kuwa hatuisaidii timu ya taifa kwa kupiga kelele zisizo na msingi, tutambue ukweli tufanye kazi kulekebisha matatizo yaliyopo katika taifa. Sio lazima wote tuwe makocha wa timu ya Taifa, tunaweza kutoa mchango kwa Taifa kwa kulea vipaji hata katika maeneo tunayoishi.

Mbona sijaona kampeni za watu kumpongeza Maximo pale timu inapofanya vizuri? Ina maana toka apewe timu hajawahi kufanikiwa? au tunafumbia macho mafanikio na kuangalia matatizo?

Comments

Popular posts from this blog

Mimi na marafiki

Picha hii ilipigwa pale uwanja wa bandari Tandika nikiwa na wakongwe James Kisaka(aliyesimama kushoto ) na Seifdin Kabange (Jezi nyekundu na white strips). Hii ilikuwa baada ya mazoezi ya Veterans wa NBC United

Dar Young Africans Vs Simba Sports club

Tommorow (saturday 31/10/2009) is one of the big days in Tanzanian Soccer. Tanzania's soccer giants Yanga (young Africans) and Simba will clash at the National stadium in Dar es Salaam. The match is expected to attract many spectators than usual, we expect revenue collections to be high. Actually we look forward to watching this big event. In the midst of expectation I can not stop myself from wondering what actually will happen tommorow. I wish to very advanced soccer tactics from the big teams, I wish to hear from TFF that they have collected as much as they expected as gate collection, I wish to see fair officiating of the match. I wish to mature and fair behavior from fans, i wish for a lot good things to happen. But I know one thing for sure: It is possible that I wont see any of my wishes coming true. It is possible to hear from TFF saying that they run deficit from the match collection. We may end up seeing the usual none fair play game from players, players from each team m...

PURPOSE OF DIFFERENT TACTICAL EXERCISES IN SOCCER

Dear readers I would like to take this opportunity to appologize for not updating information on this site for such long time. Today I just want to highlight purposes for some tactical exercises 2v1 ONE ACTS, ONE SUPPORTS, IN ATTACK OR WHEN DEFENDING. IN ATTACK, PLAYER WITH THE BALL COMMITS THE LONE DEFENDER THEN EITHER GOES PAST THEM OR PASSES TO THE SECOND ATTACKER. IN DEFENSE, NEAREST CHALLENGES, THE OTHER COVERS 3v1 IN DEFENSE, ONE CHALLENGES, ONE COVERS, THE THIRD BALANCES IN ATTACK, ONE COMMITS AN OPPONENT, ONE POSITIONS TO RECIEVE A POSSIBLE PASS, THE THIRD MAKES AN ATTACK RUN 4v2 DEFENDING - IS ABOUT THE 2 WORKING AS A PAIR TO CUT DOWN QUICKLY ANY POSSIBLE EASY SPACE FOR THE OPPONENT WITH THE BALL TO PASS TO ONE OF THE OTHER THREE ATTACKERS ATTACKING - IS ABOUT THE PLAYER WITH THE BALL HAVING THREE OPTIONS TO PASS IF THEY WISH TO (SUPPORT, PASS OPTIONS) 5v2 AS c. ONLY DEFENDING BECOMES MORE OF A POSITIONING TO FORCE THE BALL TO WHERE YOU CAN ATTACK IT FOT ATTACKING ITS ABOU...