
Nimekuwa mfuatiliaji wakaribu sana wa mjadala uliopo kati ya wapenzi wa soka,pale linapokuja suala lakuzungumzia nafasi ya golikipa wa timu ya Taifa.
Katika hilo niliamua kufuatilia magoli ambayo Ivo Mapunda amekuwa akifungwa;kwa magoli hayo utaweza kuelewa kwamba kijana huyuhana bahati na wapenzi wa timu ya taifa.
Nayaongea haya nikikumbuka magoli aliyofungwa na Msumbiji,Ghana, pamoja na yale ya Kameruni.
Ingawa magoli haya alilaumiwa Ivo, lakini yanaonyesha wazi safu ya ulinzi ya stars ilivyo na matatizo katika marking na covering. kosa hilo haliwezi kumalizwa na Ivo, waalimu wa timu pia wangelaumiwa kama wapenzi wa soka wanaogopa kuwalaumu moja kwa moja walinzi wa timu yetu hii ya Taifa.
Nimeiweka picha hii iliyopigwa na magid mjengwa makusudi ili muweze kuona mahali alikotoka mfungaji bila marking hadi anapiga free header. Kwa nini hatujiulizi mtu wa kumkaba huyu alikuwa wapi? au kwa kuwa ni kipa alitakiwa kukabwa na kipa mwenzie (IVO)?
Angalia picha kwa umakini kama ni mtu unayeijua soka utajua wazi kuwa IVO hakustahili lawama katika goli hili
Comments
Post a Comment