Skip to main content

Yanga Vs Al akhdar

Ni wazi kuwa wapenzi wa timu ya Yanga ya Tanzania watakuwa wamesononeshwa sana na kufungwa kwa timu yao. Ni ukweli usipingika kuwa katika soka lolote laweza kutokea. Kwa upande wangu niliweza kuyaona haya machache.

Al Akhdar waliifanya home work yao vizuri. ni wazi kuwa walitumia vema mchezo uliochezwa kwao Libya kufanya Match analysis. Ninasema hivyo kutokana na jinsi walivyoweza kudhibiti uchezaji wa Yanga kama timu na ule wa mchezaji mmoja mmoja.

Kwa upande wa wachezaji ilionyesha wazi kuwa waliweza kutambua uchezaji wa wachezaji kama Mrisho Ngasa, Mourice Sunguti, na Abdi Kassim.

Nikitolea mfano wa Ngasa; ni wazi kuwa walijuwa vema kwamba Ngasa ni mchezaji mwenye speed na mwenye uwezo mkubwa wa kupiga chenga na kutoa pasi nzuri. Wao waliweza kutengeneza mfumo wa kumkaba Ngasa asiweze kufanya haya yote. Katika kumkaba Ngasa walitumia wachezaji wawili, mmoja akitangulia mbele kumzuia kwa karibu (committing) na wapili alikuwa aki support kwa nyuma. pindi Ngasa akifanikiwa kumpita huyu wa kwanza huyu wa pili anafiaka kwa haraka sana kuuondoa mpira ule(walifanikiwa katika hili kwa vile walikuwa wakiitumia vema ile concept ya kuwa wa kwanza kwenye mpira-Being first to the ball).

Katika hili la Ngasa kilichotakiwa kufanyika ni either Ngasa kwa vile ni mwepesi na ana mbio,kutumia uwezo wake wa kutoa na kupokea pasi. Alitakiwa asijaribu tena kupiga chenga bali kutoa pasi kwa haraka na kufungua tena ili apewe pasi tena. Hilo kama lingeshindikana angejaribu pia kuhamia upande wa pili,kutoka kulia kwenda kushoto na kujaribu mbinu zote mbili tena. Hili lingeshindikana Kocha angemtoa na kuingiza mtu mwingine mwenye mchezo tofauti na ule wa Ngasa.

Walijua pia kuwa Abdi Kassim ni mpigaji mzuri wa Mashuti hawakumpa nafasi Abdi kupiga mashuti mara kwa mara. Kushindwa kutumia vema mguu wa kulia ni jambo pia linalomkwamisha sana Abdi.

Pengo la Nsajigwa liliweza pia kuonekana kama ukiufananisha uchezaji wa Mbuna na Nsajigwa. Wote wana Nguvu na uwezo wa kupanda, lakini nsajigwa anasaidia sana katika mashambulizi kuliko Mbuna. nsajigwa huweza kutoa krosi nzuri ambazo mara nyingi zimekuwa zikitumiwa vema na wafungaji wa Yanga na hata wale wa timu ya taifa. Mbuna alikuwa na haraka na pasi zake nyingi kupotea.

Al Akhdari waliweza kutumia mipira mirefu ya pembeni hivyo kuwakwepa Yanga waliokuwa wengi kati kati na wachache pembeni nyuma. Hili linatokana na mfumo wanaotumia yanga hivyo kuwa na mapengo katika full backs.

Athman Idd alijitahidi kuleta uhai lakini anahitajika sana kufanyia mazoezi upigaji wa penetrating passes,Idd ameonekana mwenye control nzuri, nguvu na speed. Anapiga vizuri sana square passes lakini ana tatizo katika kutoa penetration(passes).

Al akdhar walijua wazi kuwa Yanga wana nguvu na hivyo kujitahidi sana kutopoteza nguvu yao katika kipindi cha kwanza.

Ninaweza kusema kilichowafunga yanga ni maandalizi na zaidi usomaji wa mchezo wao wa kwanza uliofanyika Libya. Ni wazi wenzao waliutumia vema kuliko yanga wenyewe.

Comments

Popular posts from this blog

Mimi na marafiki

Picha hii ilipigwa pale uwanja wa bandari Tandika nikiwa na wakongwe James Kisaka(aliyesimama kushoto ) na Seifdin Kabange (Jezi nyekundu na white strips). Hii ilikuwa baada ya mazoezi ya Veterans wa NBC United

Dar Young Africans Vs Simba Sports club

Tommorow (saturday 31/10/2009) is one of the big days in Tanzanian Soccer. Tanzania's soccer giants Yanga (young Africans) and Simba will clash at the National stadium in Dar es Salaam. The match is expected to attract many spectators than usual, we expect revenue collections to be high. Actually we look forward to watching this big event. In the midst of expectation I can not stop myself from wondering what actually will happen tommorow. I wish to very advanced soccer tactics from the big teams, I wish to hear from TFF that they have collected as much as they expected as gate collection, I wish to see fair officiating of the match. I wish to mature and fair behavior from fans, i wish for a lot good things to happen. But I know one thing for sure: It is possible that I wont see any of my wishes coming true. It is possible to hear from TFF saying that they run deficit from the match collection. We may end up seeing the usual none fair play game from players, players from each team m...

PURPOSE OF DIFFERENT TACTICAL EXERCISES IN SOCCER

Dear readers I would like to take this opportunity to appologize for not updating information on this site for such long time. Today I just want to highlight purposes for some tactical exercises 2v1 ONE ACTS, ONE SUPPORTS, IN ATTACK OR WHEN DEFENDING. IN ATTACK, PLAYER WITH THE BALL COMMITS THE LONE DEFENDER THEN EITHER GOES PAST THEM OR PASSES TO THE SECOND ATTACKER. IN DEFENSE, NEAREST CHALLENGES, THE OTHER COVERS 3v1 IN DEFENSE, ONE CHALLENGES, ONE COVERS, THE THIRD BALANCES IN ATTACK, ONE COMMITS AN OPPONENT, ONE POSITIONS TO RECIEVE A POSSIBLE PASS, THE THIRD MAKES AN ATTACK RUN 4v2 DEFENDING - IS ABOUT THE 2 WORKING AS A PAIR TO CUT DOWN QUICKLY ANY POSSIBLE EASY SPACE FOR THE OPPONENT WITH THE BALL TO PASS TO ONE OF THE OTHER THREE ATTACKERS ATTACKING - IS ABOUT THE PLAYER WITH THE BALL HAVING THREE OPTIONS TO PASS IF THEY WISH TO (SUPPORT, PASS OPTIONS) 5v2 AS c. ONLY DEFENDING BECOMES MORE OF A POSITIONING TO FORCE THE BALL TO WHERE YOU CAN ATTACK IT FOT ATTACKING ITS ABOU...