Ni wazi kuwa wapenzi wa timu ya Yanga ya Tanzania watakuwa wamesononeshwa sana na kufungwa kwa timu yao. Ni ukweli usipingika kuwa katika soka lolote laweza kutokea. Kwa upande wangu niliweza kuyaona haya machache. Al Akhdar waliifanya home work yao vizuri. ni wazi kuwa walitumia vema mchezo uliochezwa kwao Libya kufanya Match analysis. Ninasema hivyo kutokana na jinsi walivyoweza kudhibiti uchezaji wa Yanga kama timu na ule wa mchezaji mmoja mmoja. Kwa upande wa wachezaji ilionyesha wazi kuwa waliweza kutambua uchezaji wa wachezaji kama Mrisho Ngasa, Mourice Sunguti, na Abdi Kassim. Nikitolea mfano wa Ngasa; ni wazi kuwa walijuwa vema kwamba Ngasa ni mchezaji mwenye speed na mwenye uwezo mkubwa wa kupiga chenga na kutoa pasi nzuri. Wao waliweza kutengeneza mfumo wa kumkaba Ngasa asiweze kufanya haya yote. Katika kumkaba Ngasa walitumia wachezaji wawili, mmoja akitangulia mbele kumzuia kwa karibu (committing) na wapili alikuwa aki support kwa nyuma. pindi Ngasa akifanikiwa kumpita huyu...