Chukua kamba iliyo na urefu mara tatu ya upana wa goli. Funga upande mmoja katika nguzo mojawapo na upande mwingine katika nguzo nyingine. Ishike kamba katikati halafu tembea kuelekea katikati ya kiwanja hadi pale pembetatu itakapojitokeza na ncha ya pembe tatu ikiwa inagawa goli katikati. Ilaze kamba chini katika umbo hili la pembe tatu.
Weka mpira katika ncha ya pembe tatu. Weka mchezaji mmoja asimame nyuma ya mpira akielekeza macho golini kwa mfano wa mchezaji anayetaka kufunga. Golikipa akae katika mstari wa goli, kwa kuanzia akae katikati kabisa ya zile nguzo mbili.
Pembe tatu iliyo tengenezwa na kamba inaashiria nafasi,pembe ambazo mfungaji anaweza kupiga mashuti na kufunga. Mpira wowote utakaopigwa nje ya kamba utatoka nje ya goli.
Ni kiasi gani kipa wako anaweza kuziba eneo la pembe tatu ndilo swali lako kuu la kujiuliza na kumpima kipa wako. Angalia uwezo wake wa kufika katika kila upande, kwanza bila kutembeza miguu yake kuelekea pembeni ili kuwa katika nafasi nzuri. Ni eneo kiasi gani linabaki bila kulindwa?
Sasa mruhusu kipa wako aanza kusogea huku akifanya hivo hivyo kama mwanzo. Kila golikipa anavyosogea ndivyo pembe isiyolindwa inavyokuwa ndogo.
Angalizo:
Kwa jinsi kipa anavyosogea mbali zaidi ya goli ndivyo uwezo wake wa kuzuia mipira ya juu unavyopungua (Mf. mfungaji akichip mpira), Pia nafasi na pembe nyuma yake inaweza kutumia kama mchezaji mwenye mpira atampasia mwenzake aliye pembeni.
Baada ya hapo:
KAtika sehemu ya mwisho hamisha kamba yako kwenda pembeni, halafu fanya kama uliyo yafanya hapo mwanzo.
Kitu muhimu kwa mwalimu kufundisha:
Mahali kipa atakuwepo katika shambulizi ni katikati ya nguzo mbili na mpira.

Comments
Post a Comment