Skip to main content

Mikakati na Malengo ya mwalimu wa Soka

Habari ya kazi wapenzi wa mchezo huu wa soka. Leo hii ningependa kuandika kuhusiana na malengo ya mwalimu katika kufundisha, na namna ya ufundishaji ili kukidhi malengo hayo.

Mwalimu wa soka anayeiandaa timu yake kwa ajili ya mchezo uliyo mbele yake. Malengo yake yanaweza kuwa kushambulia zaidi au ulinzi zaidi.

Nitajaribu kuchambua malengo haya na kuangalia vitu mihimu vya kufundisha katika hali hizi mbili.

Iwapo lengo lako ni kushambulia (Attacking),basi itakubidi uazimie na kufundisha malengo haya matatu ya ushambuliaji;

Lengo la kwanza;
Andaa timu yako ili iweze kuingia katika eneo la adui (i.e the attacking third of the field. Kuna mbinu tano za kufuata ili uweze kufanikiwa katika hili;

1. Fundisha timu yako kutumia mipira mirefu itakayofika nyuma ya ngome(walinzi) wa timu pinzani.
2. Fundisha washambuliaji wako jinsi ya kukimbia mbele bila mpira (kwa lengo la kutafuta nafasi ya kupokea mpira na kufunga.
3. Wachezaji wako waweze kutoa pasi za uhakika,zinazoelekea mbele na zinazomfikia mwenzake (team mate)mguuni. Hakikisha kunakuwa na mchezaji wa kutoa msaada, kupokea pass na kutoa pasi kwenda mbele.

4. Fundisha jinsi ya kupokea pasi na kugeuka.
5. Fundisha jinsi ya kukimbia kwenda mbele wakiwa na mpira.


Lengo la Pili

Hakikisha timu yako ina maintain au ikiwezekana iongeze nguvu ya ushambuliaji pindi mapira ukiwa katika eneo la timu pinzani (third of the attacking field). Hapa pia kuna mabo matano ya kuzingatia na kufundisha.

1. Pindi nafasi inapopatikana wachezaji wapige mashuti golini.
2. Ikiwezekana washambuliaji wako washambulie huku waki-drible.
3. Inapowezekana pasi za wachezaji wako ziwe zinapita nyuma ya safu ya ulinzi ya timu pinzani.
4. Pindi nafasi inapopatikana mawinga wako wawe wepesi kupiga krosi zikazoweza kuwavuka walinzi wa timu pinzania.
5. Hakikisha team yako inaendelea kuwa compact.

Pindi timu yako itakapofanikiwa kutimiza lengo hilo la pili itafanya kazi ya kutimiza lengo la tatu kuwa rahisi zaidi.

Lengo la tatu

Hapa lengo letu ni timu iweze kufanya vizuri zaidi ya timu pinzani katika vitu muhimu vifuatazo;

1. Kupiga mashuti; Upigaji wa mashuti golini kila mara nafasi itokeapo huongeza nafasi zaidi za kupiga mashuti kwa mipira inayorudi toka goli la timu pinzani. Nafasi hizi hutokea aidha baada ya kungonga mwamba ama kuokolewa na walinzi au kipa.

2. Kupata nafasi za kupiga kona, kurusha mipira iliyotolewa na wapinzani, na mipira ya adhabu mbalimbali.

3. Nafasi za kupiga krosi

4. Uwezo wa kurudisha mipira inayopotelea katika eneo la adui (ukabaji katika eneo la ushambuliaji.

Kufikia hapo utakuwa umeweza kuinandaa timu yako iweze kucheza mchezo wa kushambulia. Kesho tutajitahidi kuangalia lengo likiwa ni kulinda zaidi (Defensive game)

Comments

Popular posts from this blog

Mimi na marafiki

Picha hii ilipigwa pale uwanja wa bandari Tandika nikiwa na wakongwe James Kisaka(aliyesimama kushoto ) na Seifdin Kabange (Jezi nyekundu na white strips). Hii ilikuwa baada ya mazoezi ya Veterans wa NBC United

Dar Young Africans Vs Simba Sports club

Tommorow (saturday 31/10/2009) is one of the big days in Tanzanian Soccer. Tanzania's soccer giants Yanga (young Africans) and Simba will clash at the National stadium in Dar es Salaam. The match is expected to attract many spectators than usual, we expect revenue collections to be high. Actually we look forward to watching this big event. In the midst of expectation I can not stop myself from wondering what actually will happen tommorow. I wish to very advanced soccer tactics from the big teams, I wish to hear from TFF that they have collected as much as they expected as gate collection, I wish to see fair officiating of the match. I wish to mature and fair behavior from fans, i wish for a lot good things to happen. But I know one thing for sure: It is possible that I wont see any of my wishes coming true. It is possible to hear from TFF saying that they run deficit from the match collection. We may end up seeing the usual none fair play game from players, players from each team m...

PURPOSE OF DIFFERENT TACTICAL EXERCISES IN SOCCER

Dear readers I would like to take this opportunity to appologize for not updating information on this site for such long time. Today I just want to highlight purposes for some tactical exercises 2v1 ONE ACTS, ONE SUPPORTS, IN ATTACK OR WHEN DEFENDING. IN ATTACK, PLAYER WITH THE BALL COMMITS THE LONE DEFENDER THEN EITHER GOES PAST THEM OR PASSES TO THE SECOND ATTACKER. IN DEFENSE, NEAREST CHALLENGES, THE OTHER COVERS 3v1 IN DEFENSE, ONE CHALLENGES, ONE COVERS, THE THIRD BALANCES IN ATTACK, ONE COMMITS AN OPPONENT, ONE POSITIONS TO RECIEVE A POSSIBLE PASS, THE THIRD MAKES AN ATTACK RUN 4v2 DEFENDING - IS ABOUT THE 2 WORKING AS A PAIR TO CUT DOWN QUICKLY ANY POSSIBLE EASY SPACE FOR THE OPPONENT WITH THE BALL TO PASS TO ONE OF THE OTHER THREE ATTACKERS ATTACKING - IS ABOUT THE PLAYER WITH THE BALL HAVING THREE OPTIONS TO PASS IF THEY WISH TO (SUPPORT, PASS OPTIONS) 5v2 AS c. ONLY DEFENDING BECOMES MORE OF A POSITIONING TO FORCE THE BALL TO WHERE YOU CAN ATTACK IT FOT ATTACKING ITS ABOU...