Skip to main content

Mikakati na Malengo ya mwalimu wa Soka- PART II

Ni matumaini yangu kuwa leo pia tupo katika mwelekeo mmoja katika jitihada za kuufamu zaidi mchezo wetu wa soka.

Jana tuliongelea mikakati na malengo pindi unapohitaji kufundisha timu yako iweze kucheza mchezo wa kushambulia zaidi. Leo tutaangalia kwa ufupi ufundishaji pale unapohitaji kuzuia zaidi.

Njia bora zaidi ya ulinzi ni kuhakikisha timu yako inaweza kuzuia/kupokonya mipira mingi tokea katika eneo la timu pinzani. Wafundishe washambuliaji wako mbinu za ukabaji pia, ili waweze kuwa ndio mstari wa kwanza wa ulinzi kwa timu yako.

Itakuwa rahisi kwako kama timu yako itaendelea kuwa "compact". Kuwa Compact kutaisaidia timu yako kutekeleza mambo muhimu yafuatayo;

1. Hii inamaanisha kuwa itakuwa rahisi kwa timu yako kumkaba na kufanikiwa kumpokonya mpira mchezaji wa timu pinzani. Hii itamzuia au kusaidia kumchelewesha mpinzani kupeleka mpira mbele kwa washambuliaji wake.

2. Mchezaji wako (mshambuliaji) anayezuia mpira au kujaribu kumkaba mchezaji wa timu pinzani,atapata msaada wa ulinzi kutoka kwa mwenzake. PIa itasaidia kufanya marking, kuzuia nafasi (Cover space).
3. Itakuwa rahisi kwa wachezaji wako kuwakaba wachezaji wa timu pinzani wanaosonga mbele kushambulia.

Uwezekano wa timu yako kufungwa utapungua iwapo, wachezaji wako wanaolinda eneo linazozunguka eneo la penati watafanikiwa kutekeleza yafuatayo;

1. Iwapo watajitahidi kuwa wa kwanza kuufikia mpira

2. Kuokoa kwa kupiga mipira ya juu inayo kwenda mbali na yenye upana.

3. Waweze kuzuia eneo la "Far post".

4. Wahakikishe hawaponkonywi na timu pinzani haimiliki mpira katika eneo la ulinzi la timu yako. Wafundishe Kuziba nafasi, watawale eneo, wafanye "marking", waweze kufuatilia move zote za wapinzani ili kuwadhibiti

Jambo la kuzinga tia ni kwa walinzi wako kujaribu kukaa kama pembe tatu (napendelea zaidi kuiita umbo la sambusa" kuzingatia mahali mpira ulipo (iwapo upo kwa adui). Haya yafanyike kwa kuzingatia mahali ulipo mpira, mahali alipo mchezaji wa timu pinzani anayeweza kupatiwa pasi au aliyelengwa kupewa pasi, na usawa wa goli lenu.

Namna watavyojipanga ndiyo itakayo wasaidia kufanya vitu hivi vitatu;

1. Kama mpira utapigwa kwenda nyuma yao, wataweza kumzidi na kufika mapema mahali mpira ulipo kuliko adui aliye karibu.
2. Kama mpira utapelekwa kwa adui aliye karibu basi hii itawasaidia kuweza kujipanga wakati mpira ukiwa bado katika mwendo.

3. Watafanikiwa kuwa katika nafasi nzuri ya kuuona mwenendo wa mpira na wachezaji wa timu pinzani wakati wote wa mchezo.

Zaidi ya yote waandae wachezaji wako kisaikolojia ili waweze kuwa makini na kuzingatia hayo yote muda wote wa mchezo.

Comments

Popular posts from this blog

Mimi na marafiki

Picha hii ilipigwa pale uwanja wa bandari Tandika nikiwa na wakongwe James Kisaka(aliyesimama kushoto ) na Seifdin Kabange (Jezi nyekundu na white strips). Hii ilikuwa baada ya mazoezi ya Veterans wa NBC United

Dar Young Africans Vs Simba Sports club

Tommorow (saturday 31/10/2009) is one of the big days in Tanzanian Soccer. Tanzania's soccer giants Yanga (young Africans) and Simba will clash at the National stadium in Dar es Salaam. The match is expected to attract many spectators than usual, we expect revenue collections to be high. Actually we look forward to watching this big event. In the midst of expectation I can not stop myself from wondering what actually will happen tommorow. I wish to very advanced soccer tactics from the big teams, I wish to hear from TFF that they have collected as much as they expected as gate collection, I wish to see fair officiating of the match. I wish to mature and fair behavior from fans, i wish for a lot good things to happen. But I know one thing for sure: It is possible that I wont see any of my wishes coming true. It is possible to hear from TFF saying that they run deficit from the match collection. We may end up seeing the usual none fair play game from players, players from each team m...

PURPOSE OF DIFFERENT TACTICAL EXERCISES IN SOCCER

Dear readers I would like to take this opportunity to appologize for not updating information on this site for such long time. Today I just want to highlight purposes for some tactical exercises 2v1 ONE ACTS, ONE SUPPORTS, IN ATTACK OR WHEN DEFENDING. IN ATTACK, PLAYER WITH THE BALL COMMITS THE LONE DEFENDER THEN EITHER GOES PAST THEM OR PASSES TO THE SECOND ATTACKER. IN DEFENSE, NEAREST CHALLENGES, THE OTHER COVERS 3v1 IN DEFENSE, ONE CHALLENGES, ONE COVERS, THE THIRD BALANCES IN ATTACK, ONE COMMITS AN OPPONENT, ONE POSITIONS TO RECIEVE A POSSIBLE PASS, THE THIRD MAKES AN ATTACK RUN 4v2 DEFENDING - IS ABOUT THE 2 WORKING AS A PAIR TO CUT DOWN QUICKLY ANY POSSIBLE EASY SPACE FOR THE OPPONENT WITH THE BALL TO PASS TO ONE OF THE OTHER THREE ATTACKERS ATTACKING - IS ABOUT THE PLAYER WITH THE BALL HAVING THREE OPTIONS TO PASS IF THEY WISH TO (SUPPORT, PASS OPTIONS) 5v2 AS c. ONLY DEFENDING BECOMES MORE OF A POSITIONING TO FORCE THE BALL TO WHERE YOU CAN ATTACK IT FOT ATTACKING ITS ABOU...