Kwa ufupi kabisa ni kuwa kosa kubwa kabisa la Yanga lilikuwa ni uzembe. Uzembe huu ulifanywa na wachezaji wa Yanga katika maeneo makuu yafuatayo; 1. Haruna Niyonzima alipaswa kujua nini cha kufanya katika kuondoa hatari pale walipokuwa wakishambuliwa. Haruna alijaribu kuweka mpira kifuani, mpira haukukaa vizuri akajaribu kumpatia Omega ambaye hakuwa mchezoni kwa wakati huo akajikuta akipoteza mpira huo. 2.Omega akafanya kosa lapili kwa kuto kuact mapema kumsumbua adui badala yake akageuka kuangalia refa kasemaje. 3. Cross ilipopigwa ikamkuta Mido hayuko marked kabisa, akapiga free header. mabeki wa kati na Nsajigwa hawakufanya kazi yao. 4. Endapo Kado ange dive kufuata mpira angeweza kuucheza mpira ule. kichwa cha Mido hakikuwa na nguvu sana, pia kilikuwa cha chini. Hakukuwa na sababu ya yeye kuusindikiza kwa macho Wachezaji wanahitaji kuchangamka