Marcio Barcellos Maximo alimaliza mkataba wake wa kuinoa Taifa stars (Timu ya soka ya taifa ya Tanzania) mwaka 2010 mwezi wa saba, baada ya kuinoa timu hiyo kwa mafanikio kwa muda wa miaka minne. Kati ya mafanikio yaliyoletwa katika soka la Tanzania na mbrazili huyu ni pamoja na kurudisha mapenzi ya wapenzi wa mpira kwa timu yao ya Taifa. Haikuwa kazi ndogo hata kidogo kwa mbrazili huyu kuifanya timu hii iwe kipenzi tena cha watanzania, ni juhudi ya hali ya juu iliyopelekea imani ya watanzania kwa timu yao kurejea tena. Na hii ilitokana na ukweli kuwa Taifa stars ikaanza kuwa mpinzani wa kweli mara inapokutana na timu mbalimbali za bara la Africa. Misingi mikuu ya filosofia ya mwalimu huyu ilikuwa katika kujenga nidhamu ndani ya timu, umuhimu wa wachezaji kuthamini kazi yao hii ikiwa ni pamoja na kuzingatia mazoezi, umuhimu wa kujenga timu ya muda mrefu. Katika kuyafanikisha haya yote Maximo aliweza si tu kwa timu yake kuonyesha mchezo mzuri uwanjani bali pia aliweza kuwatumia vijana w...