Ni swali ambalo nimekuwa nikujiuliza kwa muda mrefu sasa. Hivi Tanzania tuna wanasoka wangapi wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi? Wanacheza katika timu za daraja gani, nchi gani na kadhalika. Pia hujiuliza ni kwa nini vyombo vya habari vya nchi hii haviwazungumzii sana? Tatizo lipo wapi? Habari zao ni ngumu kupatikana, ama ni sisi hatujui kuuza products zetu? Blog hii inajipanga kwa mwaka huu wa 2012 kuanza kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya watanzania hawa na kuziripoti kwenu kupitia mtandao huu Kaa mkao wa kula
Ni mapumziko katika mechi ya kugombea ngao ya hisani. Azam Fc wanaongoza kwa goli 2-1. Goli la simba limepatikana dakika ya 42 kwa njia ya penati. Dakika ya 69 simba wanasawazisha. Azam 2 - Simba 2